
mengine, sheria hiyo itafanya wakwepa kodi kutangazwa kwenye vyombo vya habari.
Muswada huo pia unampa Mamlaka Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufanya upekuzi, kukamata, kuchukua na kuuza
mali za mlipa kodi kwa lengo la kukomboa kodi na kuzuia ukwepaji wa kodi.
Akisoma Muswada huo bungeni jana, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum alisema lengo la Muswada huo ni kuweka mfumo wa kisasa wa
usimamizi wa kodi ulio wa wazi na wenye kuleta usawa kwa kuhuisha ndani ya sheria moja, vifungu mbalimbali vya sheria za kodi vinavyohusu usimamizi na utawala wa kodi.
Waziri Salum alisema vifungu husika ni vile vinavyohusu taratibu za ulipaji wa kodi, uwekaji wa kumbukumbu, adhabu na faini mbalimbali ambazo kwa sasa zinatofautiana kwa kila sheria
ya kodi.
Akitangaza mambo muhimu yaliyozingatiwa katika
Muswada huo, Waziri huyo alisema ni pamoja na kuweka utaratibu wa kuwatangaza kwenye vyombo vya habari wakwepa kodi wote
watakaothibitika kufanya hivyo ili kupunguza makosa sugu na ya makusudi.
Mengine ni kutambua na kuzingatia mabadiliko na matumizi ya teknolojia ya habari katika utawala wa kodi sambamba na uwasilishaji wa ritani na
ulipaji kodi kielektroniki ili kurahisisha na kuongeza ufanisi katika ulipaji wa kodi.
Madhumuni mengine ni kuweka ulazima wa kuwa na Namba ya Utambulisho kwa Mlipa Kodi (TIN) ili kufanya TIN kuwa kitambulisho katika kodi zote
na pia kuweka viwango vyenye uwiano sawa wa adhabu na faini kadri ya aina na ukubwa wa makosa ya kodi kwa kila aina ya kodi inayohusika.
Waziri Salum alisema Muswada huo pia utaweka vifungu vya kuzuia ukwepaji kodi ndani ya Sheria moja badala ya kuwa na vifungu hivyo katika
sheria ya kodi kama ilivyo katika utaratibu wa sasa.
Aidha umewekwa utaratibu ambao maamuzi ya Kamishna huhusiana na vifungu vya sheria za kodi vyenye utata wa tafsiri kutumika katika kodi
zote, bila kupotosha maana iliyokusudiwa.
“Pia Muswada utawezesha kubainisha utaratibu wa kufanya pingamizi za makadirio ya kodi pamoja na maamuzi mengine ya kikodi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) iwapo mlipakodi hataridhika. “Pia itatoa fursa kwa walipakodi kuwa na washauri wa kodi
kwa kodi zote.
Fursa hii si ya lazima kwa kila mlipakodi, bali ni hiari kulingana na uelewa wa mlipa kodi kwa kuwa ni gharama kuwa na washauri wa kodi. Piabitafanya marekebisho ya sheria za kodi husika
kwa kuondoa vifungu vinavyohusiana na utawala na usimamiaji,” alisema Waziri wa Fedha.
Tofauti na miaka ya nyuma, chini ya Muswada huo, sehemu ya 11 yenye ibara ya 93 hadi 99 inahusu Mamlaka ya Kamishna Mkuu wa TRA sasa
kuruhusiwa kufanya upekuzi, kukamata, kuchukua na kuuza mali za mlipakodi kwa lengo la kukomboa kodi na kuzuia ukwepaji kodi.
Ni sehemu hiyo pia inayoweka mamlaka ya kutangaza kwenye vyombo vya habari, majina ya walipakodi watakaofanya makosa chini ya Sheria
za Kodi ikiwemo kushindwa kulipa kodi kwa wakati.
Katika maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo kwa Wizara ya Fedha, Mbunge wa Kuteuliwa, James
Mbatia (NCCR- Mageuzi) aliitaka Serikali kutumia fursa ya kutungwa kwa Muswada huo ili kuwasilisha bungeni mapendekezo ya mfumo wa usimamizi wa kodi katika sekta ya gesi na mafuta.
Chapisha Maoni