0
Mmoja ya wapiganaji wa Dola ya Kiislamu ( Islamic State)



Mkuu wa majeshi wa Marekani amesema kampeni ya miezi mitatu dhidi ya dola ya kiislamu Islamic State
imekuwa na mafanikio, lakini akaonya Marekani na washirika wake walikabiliana na ugumu pamoja
vikwazo kwa muda mrefu.

Naye Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Chuck Hagel akizungumza kwenye bunge la congress amesema
dola ya kiislamu imedhibitiwa na hivyo haiwezi kusonga mbele na maeneo mengineBimesambaratishwa japo wanaonekana kuendeleza ushawishi kwenye ukanda wa Iraq na Syria.

Mkuu wa kikosi cha majeshi ya Marekani Generali Jack Dempsey anakadiria idadi ya wanamgambo wa
dola ya kiislam kufikia 31,000. Marekani imekuwa ikifanya mashambulizi ya anga
dhidi ya kundi hilo, ambapo pia limekuwa likitoa ushauri na mafunzo kwenye majeshi kwa majeshi ya
Marekani. 


CHANZO: BBC

Chapisha Maoni

 
Top