0
URENO imeilaza bao 1-0 Armenia mjini Faro usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Kundi I kufuzu Kombe la Mataifa ya Ulaya, maarufu kama Euro 2016.

Shukrani zimuendee Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 71 kuipatia pointi muhimu nchi yake katika mbio hizo- ambalo linakuwa bao lake la 23 kwenye mechi za kufuzu za Euro na
kuweka rekodi ya mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye michuano hiyo.

Ushindi huo, unaifanya Ureno ifikishe pointi sita baada ya kucheza mechi tatu na kupanda nafasi ya pili kwenye kundi hilo, nyuma ya Denmark wanaoongoza kwa pointi zao saba za mechi nne.

Albania ina pointi nne za mechi tatu, wakati Serbia na Armenia zina pointi moja kila moja baada ya kucheza mechi tatu. Aidha, kwa mshambuliaji huyo wa klabu bingwa Ulaya, Real Madrid- Ronaldo kutokana na kufunga bao hilo pekee jana, anakuwa mchezaji
aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye
michuano hiyo ya Ulaya.

Kikosi cha Ureno kilikuwa; Patricio, Bosingwa, Pepe, Carvalho, Guerreiro, Nani/Carvalho, Moutinho, Tiago, Ronaldo, Postiga/Eder na
Danny/Quaresma.

Armenia: Berezovsky, Hovhannisyan, Haroyan, Arzumanyan, Taron Voskanyan, Hayrapetyan,
Mkrtchyan/Pizzelli, Mkhitaryan, Yedigaryan/ Sarkisov, Ghazaryan/Manucharyan na Movsisyan.

Chapisha Maoni

 
Top