0
Watumiaji wengi wa huduma ya simu za mkononi wamekuwa wakilalamikia wizi wa pesa unaofanywa na baadhi ya makampuni hayo, jana katika kikao cha Bunge Dodoma Serikali imesema
inatambua kuhusu wizi unaofanywa na baadhi ya makampuni ya simu za mkononi na kutoa tamko namna ambavyo imejipanga kukabiliana na wizi
wa aina hiyo.

Akitoa tamko hilo Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba alisema
Serikali itaanzisha kituo maalum cha
kushughulikia malalamiko hayo CCC,
kitakachokuwa kinasimamiwa na TCRA.
Akiuliza swali kuhusiana na jinsi Serikali
ilivyojipanga kukabiliana na wizi huo Mbunge wa Konde Khatib Said Haji alisema;
“Wizi huu unaofanywa na makampuni ya simu si wizi mkubwa kama ule wa ESCROW.. ni wizi mdogo mdogo unaowaibia Watanzania elfu tano
elfu tatu lakini kwa ujumla wake, Mpemba aliyeko Konde akiibiwa elfu tatu, Mnyamwezi wa Tabora
elfu mbili, Ukizijumlisha ni mamilioni ya shilingi wanaibiwa Watanzania… Leo watu hao elfu tatu elfu mbili unawaambia wapeleke malalamiko yao,
gharama hiyo umeikadiriaje hata mtu huyo akadai malalamiko ya elfu tatu..”

“Hivi serikali yenu makini imekuwa wapi muda wote mpaka kukiri kama Watanzania wamekuwa
wakiibiwa na bila wenyewe kujijua?, na bado hamna hatua mlizozichukua, ni nani aliyeko nyuma ya pazia hili la kuibia Watanzania na ninyi mkaridhia ama ni yale yaliyosemwa kama CCM ina
fund katika wizi huu..? ”- Khatib Said Haji.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba alisema;
"Napenda nikiri tatizo la wizi au dhuluma kwa wateja lipo na ndio lililopelekea tukaweka hizi kanuni ambazo zinaweka adhabu na hatua za kuchukua katika kudhibiti wizi huo.. Licha ya
utaratibu wa kawaida wa kulalamika katika makampuni ya simu, kwa sababu moja ya matakwa ya sheria ni kwamba kampuni za simu zinapaswa kuweka utaratibu wa kuhudumia wateja
wake, lakini tumebaini kwamba utaratibu huo una matatizo, unaweza ukapiga simu muda mrefu isipokelewe, unaweza kuambiwa usubiri na wakati
unasubiri kulalamika pia unakatwa..

"Kwa hiyo Serikali inafahamu hilo, pamoja na hatua tulizozichukua ni kuweka ule mtambo wa kufuatilia mawasiliano ambao moja ya kazi yake
sio kufuatilia tu mapato lakini ubora wa
mawasiliano.. Kwa kutambua kuwa makampuni ya simu haya wakati mwingine yanachelewa wakati
mwigine yanapuuza wateja, kituo hiki ambacho tunakianzisha namba zake zitasambazwa kila mtu atakuwa nayo, kwa hiyo huna haja kusafiri
kufuatilia shilingi elfu mbili elfu tatu elfu tano.

Kutakuwa na namba ambayo ni bure kupiga..” - January Makamba. “ Kila utakapopiga kulalamika utapewa namba
maalum ya lalamiko lako, na lisiposhughulikiwa hata kitengo cha kampuni ya simu kutoshughulikia lalamiko lako na yenyewe itakuwa
sababu ya makampuni hayo kuadhibiwa.. ”- January Makamba.

Chapisha Maoni

 
Top