MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Morogoro imemnyima dhamana Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa katika kesi yake ya jinai namba 128 yamwaka 2013 leo.
Kesi hiyo imesikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Marry Moyo ambaye amesema amepokea hati ya kumfutia dhamana Sheikh Ponda kutoka kwa
Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kwa mamlaka aliyonayo hivyo yeye hana mamlaka ya kuikataa hati hiyo.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Januari 26 na 27, mwaka huu itakaposikilizwa tena.
Chapisha Maoni