Baada ya kuitwanga Taifa ya Jang'ombe kwa mabao 4-0 katika mechi ya Kombe la Mapinduzi, wamefanya hivyo tena kwa Polisi Zanzibar.
Katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, Yanga ilipata mabao yake kupitia Andrey Coutinho aliyefunga mawili, Kpah
Sherman na Simon Msuva.
Yanga ingeweza kufunga mabao mengi zaidi kutokana na kuutawala mchezo, lakini mara kadhaa wachezaji wake hawakutulia kwenye umaliziaji.
Wakati mwingine Polisi Zanzibar walilazimika kucheza kibabe ili kuwapunguza kasi wachezaji
wa Yanga ambao walifunga mabao mawili kwa kila kipindi.

Chapisha Maoni