Fainali ya Mashindano ya Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, itachezwa Jumapili ndani ya Stade de France Mjini Paris Nchini France kati ya Wenyeji France na Portugal hapo Jumapili.
Portugal hawana rekodi nzuri wakicheza na France lakini hii ni Fainali na wanae Mashiny ya Magoli, Cristiano Ronaldo, Mchezaji Bora Duniani mara 3.
Lakini France wako nyumbani na
wameshatwaa Mataji majubwa hapo kwao likiwemo Kombe la Dunia Mwaka 1998 na Mwaka huu nguvu yao ya Nyumbani inaonekana dhahiri.
EURO 2016 – MFUNGAJI BORA:
-Antoine Griezmann Bao 6
-Wachezaji 6 wakiwa na Bao 3 kila mmoja wakiwemo wa Portugal, Cristiano Ronaldo na Nani, na wa France Dimitri Payet na Olivier
Giroud.
Uchambuzi wa Timu -Portugal
Kocha wa Portugal Fernando Santos
anatarajiwa kuutumia Mfumo wake
anaoupenda wa 4-4-2 ambao Kiungo chake huwa umbo la Almasi na Kikosi chake cha kwanza huwa ni kile kile.
Wasiwasi pekee kwa Portugal ni kucheza kwa Beki Pepe ambae ana maumivu yaliyomfanya
aikose Nusu Fainali dhidi ya Wales.
Ikiwa Pepe hatakuwa fiti basi Bruno Alves ataingia Kikosini kuwa patna wa José Fonte.
Ingawa Danilo alicheza vizuri na kumdhibiti Gareth Bale wa Wales kwenye Nusu Fainali
Juzi Jumatano, inatarajiwa William Carvalho atarejea kwenye Kiungo kuungana na
wenzake wa Klabu ya Sporting CP Adrien na João Mário ili kumkomboa chipukizi Renato
Sanches kuranda kwenye uwazi katikati ya Kiungo na Fowadi za France.
-France
Kocha wa France Didier Deschamps
anatarajiwa kuutumia Mfumo wa 4-2-3-1 ambao ndio ulikuwa plani kuu kwenye Mechi zao dhidi ya Iceland na Germany.
Tangu waanze kuutumia Mfumo huo kwenye
Mechi zao hizo 2, Antoine Griezmann
amefanikiwa kufunga Bao 5.
Nae Beki Samuel Umtiti alimeremeta baada
ya kuchukua namba kutoka Adil Rami
aliekuwa Kifungoni na zipo kila dalili atabakia Kikosini.
Pia Kifungo kilimkosesha namba Kiungo
Mkabaji N'Golo Kanté na anaweza pia asianze
Fainali hii labda Deschamps apate mchecheto
wa kutaka kuimarisha ngome yake ili
kumkabili Cristiano Ronaldo.
Dimitri Payet na Moussa Sissoko pia
wanatarajiwa kubakia Kikosini wakicheza nafasi za pembeni.
Katika Mechi 24 zilizopita, France imeifunga Portugal Mechi 18 Kufungwa 1 na Sare 5. -Katika Mechi 10 zilizopita, France imeshinda Mechi zote na ya mwisho ni ile ya Kirafiki Mwezi Septemba 2015 huko Lisbon ambayo
Mathieu Valbuena alifunga Bao pekee.
Katika Mechi yao ya mwisho ya Mashindano rasmi, France walishinda 1-0 kwa Bao la Penati ya Zinédine Zidane kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Dunia la Mwaka 2006.
-Mara ya mwisho kwa Portugal kuifunga
France ilikuwa ni Bao 2-0, Miaka 40 iliyopita, hapo Aprili 1975 ndani ya Parc des Princes, Paris, France kwa Bao za Nené na Marinho.
VIKOSI:
FRANCE: Lloris; Sagna, Koscielny, Umtiti,
Evra; Pogba, Matuidi; Sissoko, Griezmann, Payet; Giroud
PORTUGAL: Rui Patrício; Cédric, Pepe, Fonte, Guerreiro; William Carvalho, Adrien, João
Mário, Sanches; Nani, Ronaldo.
REFA: Mark Clattenburg [England]
Chapisha Maoni