0
Alex Ferguson ambaye ni kocha wa
zamani anasema kwamba anavyoamini
uamuzi aliouchukua Ryan Giggs wa
kuondoka Manchester United ni wa
kumpa mafanikio kutokna na kwamba
kwa sasa anatakiwa kusimama kwa
miguu yake mwenyewe. Giggs alikuwa
kocha msaidizi kwenye klabu hiyo ya
Old Traffod chini ya aliyekuwa kocha
wake mkuu, Louis Van Gaal tangu
alipotundika daruga mwaka 2014, lakini
mwishoni mwa wiki iliyopita alitangaza
kuachana na kazi hiyo ili akatafute
kibarua sehemu nyingine.
Baada ya uamuzi huo, Ferguson
anaungana na nyota wake huyo wa
zamani kwa kuamua kwenda kusaka
timu kwingine, lakini anamuonya
akisema kuwa akipata klabu bora ndio
kitakachompa mafanikio makubwa. “Ni
muda muafaka wa Ryan kusimama kwa
miguu yake mwenyewe kwa kuondoka
mahali hapo na kwenda kukabiliana na
changamoto nyingine,” Ferguson
aliiambia BBC Sport.
Giggs
“Nadhani yupo tayari kuongoza timu na
ana uzoefu mkubwa. Hatakiwi kwenda
kupeleka ujuzi wake kwenye klabu
ambayo inafukuza makocha kila baada
ya dakika mbili,” aliongeza kocha huyo
wa zamani. Alisema kuwa
analizungumza hilo kwa moyo mkunjufu
kutokana na kwamba ana imani kubwa
kwa nyota wake huyo wa zamani.

Chapisha Maoni

 
Top