vinavyojaribu kusuguana na Jeshi la Polisi
kukumbuka kuwa hilo ni jeshi, ambalo liko tayari
kutumia nguvu na rasilimali zote, kuhakikisha raia
na mali zao ni salama.
Jeshi hilo pia limesema halihitaji msaada wowote
kutoka kwa vyama vya siasa na wakihitaji
msaada, wataomba kutoka katika vyombo vingine
vya kiusalama.
Kauli hiyo imetolewa jana na Kaimu Kamishna wa
Polisi Operesheni na Mafunzo, Nsato Mssanzya,
baada ya Baraza la Vijana la Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), kudai
kuandaa vijana kwenda Dodoma kusaidia polisi
kuzuia Mkutano Mkuu wa CCM unaotarajiwa
kufanyika Julai 23 mwaka huu.
“Nawaasa vijana, watoto msisuguane na jeshi, si
busara kusuguana na jeshi, fanyeni mambo
ambayo nchi itakuwa salama, polisi itatumia
nguvu zote pamoja na rasilimali tulizonazo
kuhakikisha raia na mali zao wanabaki salama.
“Hakuna suala la kusaidia Jeshi la Polisi au nini,
sisi tunajitosheleza wenyewe, kama tutahitaji
msaada wowote katika ulinzi basi msaada huo
tutauomba kwa vyombo vingine vya ulinzi,
ambavyo vina mafunzo kama sisi na si kwa
vyama vya siasa,” alionya.
Alisema anatumia neno ‘ole’ kwa watu
watakaojaribu kuvuruga amani kwa madai ya
kusaidia kuzuia mkutano, kwamba polisi haitasita
kuchukua hatua.
Alifafanua kuwa Jeshi la Polisi halijazuia mikutano
yote ya kisiasa na kwamba limelazimika kutoa
ufafanuzi, kutokana na kuibuka kwa tafsiri tofauti
kutoka kwa vyama vya siasa na makundi ya watu,
baada ya polisi kutoa tamko Juni 7 mwaka huu la
kupigwa marufuku mikutano ya hadhara.
Mssanzya alisema hakuna sehemu yoyote tamko
hilo lilipiga marufuku mikutano ya kiutendaji na
kiutawala ya vyama vya siasa iliyofanywa kwa
mujibu wa kanuni za vyama husika.
“Ndio maana baada ya tamko lile, baadhi ya
vyama vimefanya na kupanga kufanya mikutano
ya kiutendaji na kiutawala bila kuingiliwa au
kuzuiwa na Jeshi la Polisi,” alisema Mssanzya
akitolea mfano mkutano wa Bavicha kuzungumza
na vyombo vya habari Julai 3, mwaka huu.
Alisema shughuli ya Jumuiya ya Wanafunzi wa
Vyuo Vikuu vya Chadema (Chaso) iliyopanga
kufanyika Dodoma na ule wa chama cha ACT
Wazalendo, ilizuiliwa kwa sababu ujumbe
uliolengwa katika shughuli hizo, ulikuwa wa
uchochezi na haikuwa mikutano ya kiutendaji au
kiutawala.
Hata hivyo alisema pamoja na vyama vya siasa
kuruhusiwa kufanya mikutano hiyo ya ndani, bado
jeshi hilo lina mamlaka ya kuzuia pale
itakapobainika ina lengo la kuhamasisha
uchochezi au kuharibu amani na utulivu.
Alitoa mwito kwa wananchi wote na vyama vya
siasa, kuheshimu sheria za nchi na kutoa
ushirikiano kwa jeshi hilo katika kuhakikisha
usalama wa raia na mali zake unaendelea
kuimarika.
Chapisha Maoni