0
Mchezaji straika aliyetemwa Karim
Benzema alikipongeza kikosi cha
Ufaransa kwa kufanikiwa kutinga hatua
ya fainali ya michuano ya mataifa ya
Ulaya. Staa huyo wa timu ya Real Madrid
alitoswa kwenye kikosi hicho baada ya
kufunguliwa mashitaka ya kutuma picha
chafu zinazomhusu mchezaji mwenzake,
Mathieu Valbuena.
Licha ya kuwa na staa huyo mwenye
umri wa miaka 28, kikosi hicho cha
kocha Didier Deschamps kimefanikiwa
kutinga hadi hatua ya fainali ya
michuano hiyo kikiwa kwenye ardhi yake
baada ya majuzi kuwafunga mabingwa
wa dunia, Ujerumani kwenye hatua ya
nusu fainali.
Mchezaji Karim Benzema
Kabla ya mchezo huo uliopigwa kwenye
uwanja wa Stade Velodrome uliopo mjini
Marseille, Benzema alituma ujumbe
kupitia mtandao wake wa kijamii wa
Instagram akielezea kuiunga mkono timu
hiyo ya taifa. “Japokuwa sipo nao
kimwili, lakini kiroho nipo nao na
nawatakia mechi njema,” aliandika
kwenye ukurasa huo.

Chapisha Maoni

 
Top