0
Kwa sasa dirisha la usajili kwa nchi
nyingi hasa za Ulaya limeendelea
kushika kasi kwa vilabu mbalimbali
kuendelea kuongeza wachezaji wapya
ama kupunguza kwa maana ya kuuza na
kununua. Huku hapa Tanzania napo timu
zikiendelea kujidhatiti kuliibuka taarifa
ama fununu kuhusiana na mchezaji
Mbwana Samatta anayechezea klabu ya
Genk ya nchini Ubelgiji kutakiwa
kujiunga na klabu ya As Roma ya nchini
Italia inayoshiriki ligi kuu ya nchini
humo yaani Serie A.
Hapa wakilitolea ufafanuzi suala hilo
Kwa taarifa ama fununu hizo zilionekana
kuanzia kwenye mitandao ya kijamii
yaani Twitter lakini baadaye zikasambaa
mpaka kufikia baadhi ya vyombo vya
habari baadhi kuthitibisha taarifa hizo.
Taarifa zilisema kuwa Samatta
alitegemewa kupanda ndege kwenda
kumalizana na As Roma baada ya kuwa
klabu hizo mbili zimemalizana juu ya
usajili wake.
Wakala wa Mbwana Samata, Nicholas
Onise ametoa ukweli wa mambo ambapo
alikataa kwa haraka tu na kuashiria
kuwa hakuna mazungumzo
yaliyokuwepo ama yaliyokuwa
yamefanyika kumuhusisha Samata
kuelekea nchini Italia kama ilivyokuwa
imeripotiwa awali. Onise amekanusha na
kudai kuwa Samatta ni mchezaji wa
Genk na atacheza Genk.

Chapisha Maoni

 
Top