0
Beki Hassan Kessy amerejea mazoezini
Yanga kama ilivyo kwa mshambuliaji, Obey
Chirwa raia wa Zambia.
Kessy aliamua kuacha mazoezi siku kadhaa
ili kushughulikia suala lake na klabu ya
Simba ambayo imemuwekea ngumu.
Wakati Chirwa alirejea kwao Zambia
kukamilisha mambo kadhaa ambayo
yalielezwa ni ya kifamilia.
Wawili hao, walikuwa mazoezini wakijifua
na wenzao jana jioni, wakionyesha kuwa
katika hali nzuri na tayari kwa kazi.
Chirwa na Kessy walionyesha wepesi na
kufanya wawe kivutio kwa mashabiki
waliojitokeza kuwashuhudia mazoezini.
Tayari Chirwa ameichezea Yanga mechi
moja dhidi ya TP Mazembe wakati Kessy
bado hajacheza kwa kuwa Simba bado
inaendelea kuweka ngumu kwa madai
alisaini mkataba na Yanga kabla ya ule
aliokuwa nao kwisha.

Chapisha Maoni

 
Top