0
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa
Tanzania, Mbwana Ally Samatta
ameendelea kung'ara katika klabu yake,
KRC Genk ya Ubelgiji baada ya jana
kufunga bao moja katika ushindi wa 4-0
ugenini dhidi ya Lommel United.
Nahodha huyo wa Tanzania, Taifa Stars
jana alifunga dakika ya 46 bao la tatu
katika mchezo huo wa kirafiki, baada ya
Kumordzi kutangulia kufunga la kwanza
dakika ya 33 na Bailey la pili dakika ya
35.
Aliyehitimisha karamu ya mabao ya KRC
Genk inayojiandaa na mechi za mchujo
za Europa League alikuwa ni Trossard
aliyefunga bao la nne dakika ya 68.
Kikosi cha KRC Genk jana kilikuwa; Bizot,
Walsh/Castagne dk83) Dewaest,
Kumordzi, Uronen, Ndidi, Pozuelo/Sabak
dk77), Bailey/Trossard dk45, Buffalo/
Karelis dk72, Samatta/de Camargo dk72)
na Kebano/Tshimanga dk77.
Wiki iliyopita Samatta alifunga mabao
mawili mfululizo ndani ya siku mbili
katika mechi za kirafiki pia.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba
SC, alifunga bao moja katika ushindi
wa 5-0 dhidi ya Bocholt Julai 1 na
akafunga tena bao moja katika ushindi
wa 3-0 Julai 2 dhidi ya ESK Leopoldsburg.
Mbwana Samatta ameendeleza moto wa
mabao KRC Genk baada ya ja a kufunga
katika ushindi wa 4-0

Chapisha Maoni

 
Top