0
Hafla ya kukabidhi tuzo mbalimbali za
washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara kwa msimu wa 2015/2016 itafanyika Julai 17 mwaka huu.

Jumla ya tuzo 13 za Ligi hiyo
inayodhaminiwa na kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom Tanzania
zitatolewa katika hafla hiyo itakayofanyika
jijini Dar es Salaam, na kuratibiwa na
Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF).
Kamati hiyo inaundwa na waandishi wa
habari za michezo, makocha, viongozi
(administrators) na wawakilishi kutoka kwa
wadhamini (Vodacom na Azam Tv).
Tuzo hizo ni mabingwa, makamu bingwa,
mshindi wa tatu, mshindi wa nne, timu
yenye nidhamu, mfungaji bora, mchezaji
bora wa Ligi, kipa bora, kocha bora,
mchezaji bora chipukizi, mchezaji bora wa
kigeni, goli bora la msimu na mwamuzi
bora.
Waliopendekezwa (nominees) kuwania tuzo
ya mchezaji bora wa Ligi ni Shiza Kichuya
(Mtibwa Sugar), Juma Abdul (Yanga) na
Mohamed Hussein (Simba) wakati kwa
upande wa kipa bora ni Aishi Manula
(Azam), Beno Kakolanya (Tanzania
Prisons) na Deogratius Munishi (Yanga).
Kocha bora wapo Hans Van Pluijm
(Yanga), Mecky Maxime (Mtibwa Sugar) na
Salum Mayanga (Tanzania Prisons).
Waliopendekezwa kuwania tuzo ya
mchezaji bora chipukizi ni Farid Mussa
(Azam), Mohamed Hussein (Simba),
Mzamiru Yasin (Mtibwa Sugar) na Shiza
Kichuya (Mtibwa Sugar).
Waliongia kwenye orodha ya tuzo ya
mchezaji bora wa kigeni ni Donald Ngoma
(Yanga), Thabani Kamusoko (Yanga) na
Vincent Agban (Simba). Waamuzi bora
katika kinyang'anyiro hicho ni Anthony
Kayombo, Ngole Mwangole na Rajab
Mrope.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,
Matina Nkurlu amewapongeza wateule
wote waliopendekezwa kuwania tuzo hizo.
"Kama wadhamini tuna matumaini
makubwa kuwa msisimko wa ligi hii
utazidi kuongezeka katika msimu ujao na
kuzidi kuwapatia mashabiki wa soka
wanaoifuatilia hapa nchini na nje ya nchi."
Alisema Vodacom itaendelea kudhamini
ligi hiyo kubwa ya soka nchini ili
kutekeleza moja ya malengo yao ya kuibua
na kuendeleza vipaji vya wachezaji nchini.
Pia kuwawezesha wachezaji kujipatia ajira
na kuboresha maisha yao kupitia sekta ya
michezo bila kusahau kuwapatia burudani
wateja wake na Watanzania wote kwa
ujumla.

Chapisha Maoni

 
Top