0
Kamati ya olimpiki nchini Kenya, Nock, naBBChirikisho la riadha nchini Kenya, AK, zimetaja timu itakayoiwakilisha Kenya mjini Rio, nchini
Brazil Agosti mwaka huu.
Ingawa wanariadha wawili wa kwanza katika kila
kitengo walijanyakulia tiketi, Kikosi cha Kenya pia
kimeangazia masuala mengine kama vile fomu ya
wanariadha, matokeo yao katika mbio za riadha
duniani yakiwemo mashindano ya hivi karibuni ya
riadha nchini Afrika Kusini.
Mwanariadha anayeshikilia rekodi ya Olimpiki
katika mbio za mita mia nane, David Rudisha,
amepewa fursa nyingine ya kushiriki katika
Olimpiki licha ya kubwagwa na Alfred Kipketer.
Licha ya kujiondoa kutoka mbio za mita elfu kumi,
bingwa wa Dunia, Geodfrey Kamworor ni miongoni
mwa wanariadha watakaowania medali katika mbio
hizo ifikapo Agosti. Kamworor, na Bedan Karoki
wataungana na mshindi wa mbio za majaribio Paul
Tanui, na mwenzake Charles Yosei aliyenyakua
nafasi ya pili.
"Ninafuraha kubwa kuiwakilisha Kenya Katika
Olimpiki. Natarajia nitafanya vyema katika
mashindano ya Olimpiki," alisema Tanui.
Katika mbio za mita mia nane, upande wa kina
dada, mshindi wa mbio za majaribio Margaret
Nyairera Wambui, anatarajia ushindani mkali
kutoka Eunice Sum, na Winnie Chebet wakati
watakapokutana kwenye olimpiki licha ya
kuwabwaga katika mbio za majaribio.
Hata hivyo Kenya inatarajia ushindani mkali kutoka
kwa Caster Semenya.
"Ni majivuno makubwa kufuzu na naamini hakuna
mtu asiyeweza kushindwa, nia yangu ni kuondoka
na dhahabu, alisema mshindi wa mbio za
majaribio, Margaret Nyairera.''
Kwa upande wa mbio za mita mia nne kuruka
vihunzi, bingwa wa dunia Nicholas Bett na pacha
wake, Aaron Koech waliitwa kwenye timu hiyo.
Kujumuishwa kwa Bett kuliwashangaza wengi
kwani hakushiriki kwenye majaribio.
Bingwa wa mbio za mita elfu tano na elfu kumi
upande wa wanawake, Vivian Cheruiyot, alitajwa
katika timu zote mbili ambapo analenga kuwania
katika vitengo vyote viwili.
Wengine waliotajwa ni mrusha mkuki, Julius Yego,
ambaye atakuwa mwakilishi pekee wa Kenya katika
mashindano ya Rio.
''Tunawapongeza wote waliofuzu, na wakati huu
tunatarajia kujiandaa ipasavyo ili kufanya vyema
katika mashindano ya Rio," alisema rais wa riadha
nchini Kenya, Jackson Tuwei.

ORODHA KAMILI - WANAUME 200m: Kevin
Nkanata, Mike Mokamba 400m Hurdles: Nicholas
Bett, Boniface Mucheru, Aron Koech 400m: Alphas
Kishoyan, Raymond Kibet, Alex Sampao, Boniface
Mweresa 800m: Alfred Kipketer, Ferguson Rotich,
David Rudisha 1500m: Asbel Kiprop, Elijah
Manangoi, Ronald Kwemoi 3000m S/Chase:
Brimin Kipruto, Conceslus Kipruto, Ezekiel Kemboi
5000m: Caleb Mwangangi Ndiku, Isaiah Kiplangat
Koech 10000m: Paul Tanui, Charles Yosei, Geoffrey
Kamworor, Bedan Karoki Marathon: Eliud
Kipchoge, Stanley Biwott, Wesley Korir Kurusha
mkuki: Julius Yego Kutembea 20km: Samuel
Gathimba, Simon Wachira High Jump: Mathew
Sawe

ORODHA KAMILI WANAWAKE 400m Hurdles:
Maureen Jelagat 400m: Maureen Jelagat, Margaret
Nyairera Wambui 800m: Margaret Nyairera
Wambui, Eunice Sum, Winnie Chebet, 1500m: Faith
Chepngetich, Nancy Chepkwemoi. Viola Lagat
3000m S/Chase: Hyvin Kiyeng, Beatrice
Chepkoech, Lydia Rotich 5000m: Vivian Cheruiyot,
Hellen Obiri, Mercy Cherono 10000m: Vivian
Cheruiyot, Betsy saina, Alice Aprot
Marathon:Jemima Sumgong, Helah Kiprop, Visline
Jepkesho Kutembea 20km: Grace Wanjiru




BBC

Chapisha Maoni

 
Top