michuano ya kuwania Kombe la Shirikisho Barani
Afrika, timu ya mpira wa miguu ya Medeama
kutoka Ghana, itawasili Dar es Salaam, Tanzania
Alhamisi Julai 14, 2016 kwa ndege ya Shirika la
Ndege la Kenya (KQ), imefahamika.
Young Africans itaikaribisha Medeama ikiwa ni
mchezo wa tatu kuwania taji hilo hatua ya
makundi. Mchezo utafanyika saa 10.00 jioni
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Julai 16, mwaka
huu.
Huu ni mchezo wa tatu kwa Young Africans katika
harakati za kuwania Kombe la shirikisho hatua ya
makundi. Michezo miwili ya awali ilikuwa ni dhidi
ya Mo Bejaia ya Algeria ambako ilipoteza kwa bao
1-0 kabla ya kupoteza tena dhidi ya TP Mazembe,
mechi iliyopigwa jijini Dar es Salaam.
Mchezo wa Jumamosi utachezeshwa na waamuzi
kutoka Misri ambao ni Ibrahim Nour El Din
atakayekuwa mwamuzi wa kati; akisaidiwa na
Ayman Degaish na Samir Gamal Saad wakati
mwamuzi wa akiba akiwa ni Mohamed Maarouf
Eid Mansour.
Kamishna wa mchezo huo atakuwa Pasipononga
Liwewe kutoka Zambia na maofisa wasimamizi ni
Mfubusa Bernard ambaye atasimamia utendaji wa
waamuzi wakati Mratibu Mkuu wa mchezo huo
kutoka CAF atakuwa Ian Peter Keith Mc Leod.
Chapisha Maoni