0
Kwa habari kutoka kwa wakili wa nyota
Lionel Messi na baba yake Jorge,
amesema kuwa watakata rufaa kupinga
adhabu ya kifungo cha miezi 21
walichopewa wateja wake baada ya
kutiwa hatiani kwa kosa la ukwepaji
kodi. Hatua hiyo imekuja baada ya nyota
huyo wa Barcelona, Messi kutiwa hatiani
na mahakama ya Hispania kwa kosa la
kukwepa kodi ya euro milioni 4.1 katika
kipindi cha kati ya mwaka 2007 na
2009.
Inaonekana Messi hawezi kutumikia
kifungo hicho kutokana na kwamba kesi
hiyo imekwishaunguruma kwa muda wa
miaka miwili na kwa mujibu wa sheria
za Hispania, adhabu hiyo inaweza
ikafutwa. Kutokana na hali hiyo, wakili
wa Messi amesema kuwa anavyoona
kesi hiyo ni ya uzushi na huku akisema,
wateja wake hawana hatia na akasema
kuwa ataendelea kupambana dhidi ya
uamuzi huo.

Chapisha Maoni

 
Top