0
Ili kuendelea kubaki Miami Heat,
mchezaji wa kikapu wa klabu ya Miami
Heat nchini Marekani, Dwyane Wade
ametaka mkataba mwingine ili kuendelea
kubaki na miamba hiyo. Nyota huyo
ambaye ameshiriki mara 12 NBA All
Star, anawaniwa na Chicago Bulls na
Denver Nuggets; endapo Miami Heat
hawatakubali kumpa mkataba mwingine
wenye donge nono.
Ni kwamba kwa miaka miwili ijayo Miami
wanaweza kutoa kitita cha dola milioni
40 kwa nyota huyo kubaki klabuni hapo,
huku Wade akisisitiza kutaka mkataba
mrefu. Bulls walikuwa na mazungumzo
ya ana kwa ana na nyota huyo, huku
wakishindwa kufikia muafaka. Chanzo
kimoja kimesema Wade mwenye miaka
34, ana furaha na ofa ndogo iliyotolewa
na Miami Heat ambao wamekuwa na
matarajio ya kumsajili Hassan Whiteside,
huku wakimfukuzia mshambuliaji Kevin
Durant.
“Wade ameshika chati katika soko nchini
humo na ndio sababu klabu nyingi
zinawania saini yake,” kilisema chanzo
kimoja nchini humo. Mzaliwa huyo wa
Illinois amekuwa mahiri katika NBA hadi
kuwa kinara wa mauzo ya jezi yake
tangu mwaka 2005 hadi katikati ya
msimu wa 2016/17!

Chapisha Maoni

 
Top