Nyota wa klabu ya Barcelona, Neymar
amesikitishwa na jinsi anavyochukuliwa
na vyombo vya habari kutokana na
kuhusika katika kesi mbalimbali akisema
kuwa vinamuonea kutokana na kuwa
yeye si muhalifu. Uhamisho wa straika
huyo kutoka Santos na kwenda kujiunga
na klabu hiyo ya Camp Nou mwaka
2013 hadi sasa unakabiliwa na sakata la
kisheria nchini Hispania na Brazil
ambapo Neymar na baba yake
wanadaiwa kukwepa kodi. Katika sakata
hilo, mapema Februari mwaka huu,
mahakama kuu ya Sao Paul iliamuru
mali za nahodha huyo wa timu ya taifa
ya Brazil zenye thamani ya euro milioni
45 zitaifishwe.
Mwezi Juni klabu ya Barca ilikubali
kulipa faini ya euro milioni 5.5 kwa ajili
ya kufunga hatua za kisheria nchini
Hispania, lakini kesi ya mjini Sao Paul
imeendelea kuwa wazi, lakini Neymar
anasema ana uhakika mambo hayo
yatamalizika hivi karibuni. “Sijawahi
kufanya kitu chochote kinyume cha
sheria, mimi sio mhalifu,” Neymar
aliuambia mtandao wa Isto E. “Kwa
bahati mbaya, baadhi ya watu
wamekuwa wakijaribu kuzua utata.
Sifahamu kama wanashindwa kupata
taarifa sahihi,” aliongeza nyota huyo.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni