0

Wapinzani wa klabu ya Young Africans, katika
michuano ya kuwania Kombe la Shirikisho Barani
Afrika, Medeama kutoka Ghana, wametua Dar es
Salaam tayari kwa mechi baina ya timu hizo
Jumamosi.
Wachezaji hao waliwasili Dar Alhamisi na
wakafanya mazoezi katika uwanja wa Karume.
Yanga itaikaribisha Medeama kwa mchezo wa tatu
kuwania taji hilo hatua ya makundi katika uwanja
wa taifa Dar es Salaam.
Mchezao huo utaanza saa 10.00 jioni
Michezo miwili ya awali ya Yanga katika michuano
hiyo ilikuwa ni dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria
ambako ilipoteza kwa bao 1-0 kabla ya kupoteza
tena dhidi ya TP Mazembe, mechi iliyopigwa jijini
Dar es Salaam.
Mchezo wa Jumamosi utachezeshwa na waamuzi
kutoka Misri ambao ni Ibrahim Nour El Din
atakayekuwa mwamuzi wa kati; akisaidiwa na
Ayman Degaish na Samir Gamal Saad wakati
mwamuzi wa akiba akiwa ni Mohamed Maarouf Eid
Mansour, kwa mujibu wa Shirikisho la Kandanda la
Tanzania (TFF).




Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top