RAIS wa Jamhuri ya Rwanda Mhe. Paul
Kagame akiwa tayari kukabidhi tuzo kwa
Wizara, taasisi za Serikali, kampuni, nchi
washiriki pamoja na mashirika
yaliyoshinda katika maonesho ya 40 ya
biashara ya kimataifa katika uwanja wa
maonesho wa Mwalimu Nyerere barabara
ya Kilwa jijini Dar es salaam Ijumaa Julai
1, 2016. Kushoto kwake ni mwenyeji wake
Rais Dkt John Pombe Magufuli na kulia
kwake ni Waziri wa Viwanda,Biashara na
Uwekezaji Mhe. CharlesMwijage akifuatiwa
na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade,
Bw. Edwin Rutageruka.
Rais Paul Kagame alikabidhi tuzo hizo
Ijumaa Julai 1, 2016 wakati alipokuwa
akifungua maonesho ya 40 ya biashara ya
kimataifa katika viwanja vya Mwl Nyerere
maarufu kama Sabasaba, vilivyopo katika
barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
Wizara na taasisi za Serikali, kampuni
pamoja na mashirika mbalimbali yalishiriki
maonesho hayo kwa kushindana katika
kuonesha bidhaa bora na kueleza huduma
nzuri wanazotoa, ambapo baadae Rais
Paul Kagame aliwakabidhi washindi hao
tuzo mbalimbali.
Baadhi ya washindi hao walioganywa
katika makundi mbalimbali ni pamoja na,
kundi la bidhaa za kilimo nafasi ya
mshindi wa tatu ilishikwa na kampuni ya
farm equip Tanzania limited, nafasi ya
mshindi wa pili ilishikwa na kampuni
Asas dairies na nafasi ya mshindi wa
kwanza ilishikwa na Shirika la Uzalishaji
Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT).
Katika kundi la usindikaji wa vyakula na
huduma za vinywaji, nafasi ya mshindi wa
tatu ilishikwa na kampuni ya Bakhresa
Group, ikifuatiwa na kampuni ya P&P, na
nafasi ya mshindi wa kwanza ilishikwa na
kampuni ya Afri tea and coffe blenders
limited.
Kwa upande wa taasisi za kifedha, nafasi
ya mshindi wa tatu ilishikwa na benki ya
TIB, ikifuatiwa na Benki ya CRDB huku
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ikishika
nafasi ya kuwa mshindi wa kwanza.
Vilevile katika kundi la Mifuko ya hifadhi
ya jamii nafasi ya mshindi wa tatu
ilishikwa na mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya
Jamii wa NSSF, nafasi ya mshindi wa pili
ilishikwa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF
na nafasi ya mshindi wa kwanza ikiwa ni
Mfuko wa Pensheni wa PPF.
Kwa upande wa nchi za kigeni zilizoshiriki
maonesho hayo ya 40 tuzo zilienda kwa
nchi za Rwanda iliyoshika nafasi ya
mshindi wa tatu, Ujerumani ikishika nafasi
ya mshindi wa pili huku nafasi ya mshindi
wa kwanza ikiwa ni nchi ya Afrika
Kusini. Aidha, washindi wa jumla
walioshiriki katika maonesho ya 40 ya
biashara ya kimataifa ya Sabasaba ni Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
kilichoshika nafasi ya mshindi wa tatu ,
ikifuatia Wizara ya Maliasili na Utalii
pamoja Chuo cha Cha Ufundi Stadi (VETA)
kilichoshika nafasi ya mshindi wa kwanza.
Baada ya kuwakabidhi tuzo hizo na
kufungua rasmi maonesho hayo ya 40 ya
biashara ya kimataifa Rais Kagame alitoa
wito kwa washiriki wa maonesho hayo ya
40, kushirikiana ili kubuni mawazo mapya
ya biashara ikiwa ni pamoja na kutambua
fursa zilizopo katika soko la pamoja la
Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, katika
kukuza biashara zao na kusaidia ukuzaji
wa uchumi wa pamoja katika nchi
wanachama wa Jumuiya hiyo.

posted from Africa Newss
Chapisha Maoni