ya kuingia Mkataba na kocha
Mcameroon Joseph Marius
Omog sasa imehamia
kwenye kusajili wachezaji
bora wa kigeni.
Wakati tayari ikiwa imefikia
makubaliano na
mshambuliaji wa kimataifa
wa Burundi, Laudit Mavugo
aje kusiani Mkataba wa
miaka miwili, Simba SC
inaleta mshambuliaji hatari
kutoka Ivory Coast.
Huyo ni Goue Frederic Noel
Blagnon aliyezaliwa Desemba
26, mwaka 1985 ambaye
anatokea klabu ya African
Sports ya kwao, Ivory Coast.
Goue Frederic Noel Blagnon
akimiliki mpira ya wachezaji
wa timu pinzani wakati
anacheza Asante Kotoko ya
Ghana
Mchezaji huyo wa zamani wa
Union Sportive de Bitam ya
Gabon na Asante Kotoko ya
Ghana, anakuja Simba SC
kwa msaada wa kipa Muivory
Coast wa timu hiyo, Vincent
Angban.
Blagnon anayependa kuvaa
jezi namba 11, anatarajiwa
kuwasili usiku huu pamoja
na kipa Angban na Jumatatu
anaweza kuwa mazoezi
Simba SC, ili kwanza kocha
Omog amuone na
kujiridhisha juu ya uwezo
wake.
Omog alisaini Mkataba wa
miaka miwili Ijumaa, ikiwa ni
siku moja baada ya kuwasili
nchini na anarithi mikoba ya
Muingereza Dylan Kerr
aliyetimuliwa mapema
mwaka huu na nafasi yake
kukaimishwa Mganda
Jackson Mayanja.
Ingawa Simba SC inataka
Mayanja aendelee na kazi
kama Msaidizi wa Omog,
lakini hakuna uhakika kama
hilo litawezekana na tayari
taarifa zisizo rasmi zinasema
Mganda huyo anataka
kurejea Kagera Sugar.
Simba SC inatarajiwa kuanza
mazoezi Jumatatu na
wachezaji kadhaa wapya
wanatarajiwa kuhudhuria ili
kufanyiwa majaribio.
Chapisha Maoni