Katika jitihada za kukihami kikosi chao kabla ya kutetea taji lao, Mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza Leicester City wamemsajili kiungo cha
kati wa Ufaransa Nampalys Mendy.
Mchezaji huyo zamani akiichezea klabu ya Nice ametia sahihi mkataba wa miaka minne kufanya shughuli nchini Uingereza.
Hata hivyo, Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 hajawahi kuitwa katika kikosi cha taifa cha
Ufaransa.
Hadi tulipochapisha habari hizi haikuwa imebainika
mkataba huo ni wa kitita cha pesa ngapi.
Mendy alijiunga na Nice mwaka wa 2013 akitokea
klabu ya Monaco alikoichezea katika mechi 110 za
ligi ya daraja ya juu Ligue 1 katika misimu 3.
Mendy ni mchezaji wa tatu kujiunga na Leicester
baada ya kipa Ron-Robert Zielerand na mlinzi Luis
Hernandez.
Chapisha Maoni