0
Manchester United wamewaambia Juventus kuwavwako tayari kulipa pauni milioni 100 kumsajili kiungo kutoka Ufaransa Paul Pogba, 23, na
watampa mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki
(Mail on Sunday), Arsenal watampa mkataba mpya Arsene Wenger kwa matumaini ya kumshawishi
asiondoke baada ya tetesi kuzagaa kuwa chama
cha soka cha England, FA, kinamnyatia (Observer), meneja mpya wa Manchester City, Pep Guardiola anataka kumsajili mshambuliaji kutoka Uruguay
anayeichezea Barcelona, Luis Suarez, 29,
anayedhaniwa kuwa na thamani ya pauni milioni 85, pamoja na kiungo Mjerumani anayechezea Real
Madrid, Toni Kroos, 26, ambaye kipengele chake
cha uhamisho kina thamani ya pauni milioni 63 (Sunday Mirror), mabingwa wa Ufaransa Paris St-
Germain wamekubali kumsajili kiungo kutoka
Poland anayechezea Sevilla Gregorz Krychowiak,
26, kwa pauni milioni 22 (Marca), Liverpool
watapambana na Everton katika kumsajili kiungo
kutoka Ubelgiji Axel Witsel, 27, anayecheza soka
Zenith St Petersburg nchini Urusi (Sunday Mirror),
mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na
Arsenal, Robin van Persie, 32, huenda akarejea
katika Ligi Kuu ya England baada ya klabu yake ya
sasa Fernabahce ya Uturuki kuwaambia West Ham
na Crystal Palace kuwa wanaweza kumsajili (Sun
on Sunday), Chelsea wamefanikiwa juhudi za
kumsajili beki kutoka Senegal, Kalidou Koulibaly,
25, anayechezea Napoli kwa pauni milioni 30
(Sunday Mirror), Tottenham wanajiandaa kutoa
pauni milioni 38, kumtaka mshambuliaji wa Inter
Milan, Mauro Icardi, 23, na tayari wamepeleka
wawakilishi wao Italy kuzungumza na mchezaji
huyo kutoka Argentina (GianlucaDiMarzio), kipa wa
Spurs Hugo Lloris, 29, ananyatiwa na Real Madrid
kwa pauni milioni 35 (Sunday Mirror), meneja wa
Tottenham Mauricio Pochettino yuko tayari
kumuuza Ryan Mason, 25, kwenda Hull City
iliyopanda daraja kwa pauni milioni 10 (Sun on
Sunday), kiungo wa Watford Jose Manuel Jurado,
30, amehusishwa na kuhamia Espanyol na
kuungana na meneja wake wa zamani Quique
Sanchez Flores (Fichajes), Middlesbrough
watakamilisha usajili wa pauni milioni 11.75 wa
kiungo kutoka Atalanta, Marten de Roon, 25, baada
ya kukubaliana maslahi binafsi na mkataba wa
miaka minne (Gazette), timu nne za EPL zimekuwa
zikiwasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa
Wales, Hal Robson Kanu tangu alipopachika bao
dhidi ya Ubelgiji kwenye michuano ya Euro 2016.
Kanu ni mchezaji huru baada ya kuachiliwa na
klabu yake ya Reading (Sky Sports), Stoke huenda
wakalazimika kulipa takriban pauni milioni 20 kama
wanataka kumsajili mshambuliaji wa West Brom,
Saido Berahino, 22 (Stoke Sentinel). 




















Chz
@Kikeke

Chapisha Maoni

 
Top