Kiungo wa zamani wa Arsenal, Mikel Arteta amepewa kazi ya ukocha chini ya meneja mpya wa
Manchester City, Pep Guardiola. Arteta, 34, alistaafu kucheza soka msimu uliopita baada ya
kuwepo Emirates kwa miaka mitano. Alishinda
makombe mawili ya FA akiwa na Arsenal, baada
kucheza mechi 150 na kufunga magoli 17.
"Ukocha ni jambo ambalo nimekuwa nikitaka
kufanya," amesema Arteta ambaye ameelezea
nafasi ya kufanya kazi na Guardiola kama "nafasi
nzuri sana".
Posted Africa Newss
Chapisha Maoni