0
Watu 9 wamekufa na wengine 36 wamenusurika katika Mto Ruvuma wakati wakivuka mto Ruvuma
kutoka Mkenda wilayani Songea kwenda Mitomoni wilayani Nyasa baada ya mtumbwi waliokuwa
wamepanda kupinduka.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Binilith Mahenge akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya
mkoa ametembelea eneo la tukio mpakani mwa
Tanzania na Msumbiji na kutoa pole kwa
waliopatwa na msiba huo ambapo serikali imetoa
rambirambi ya shilingi laki mbili kwa kila familia iliyofiwa
Diwani wa kata ya Mitomoni wilayani Nyasa
Bw.Hamis Mbegu amesema miilii ya watu
waliokufa ambao wote ni wakazi wa kata hiyo bado
haijapatikana na vifaa vya uokoaji bado ni changamoto ingawa jitihada bado zinaendelea za
kutafuta miili hiyo ambapo wananchi wametega
nyavu kwenye mto Ruvuma ili kuinasa.





ITV

Chapisha Maoni

 
Top