Henrikh Mkhitaryan, 27, atakamilisha uhamisho kutoka Borussia Dortmund kwenda Manchester United weekend hii. Mchezaji huyo kutoka Armeniaatagharimu takriban pauni milioni 26 (Daily Mail),
Manchester City wapo tayari kulipa hadi pauni milioni 50 kumsajili beki John Stones, 22, kabla ya
kuanza kwa mechi za kabla ya msimu (Telegraph),
Crystal Palace wamekubali kulipa pauni milioni 12.5 kumsajili beki wa West Ham James Tomkins,
27 (Daily Mail), mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wanafikiria kumsajili beki wa kati wa
Arsenal Laurent Koschielny, 30, ambaye mkataba
wake Emirates unamalizika mwaka 2019 (Evening
Standard), Everton wamekubali kumsajili kiungo wa
Ubelgiji Axel Witsel, 27, kutoka Zenith St
Petersburg na watamlipa mchezaji huyo zaidi ya pauni 100,000 kwa wiki (Squawka), Stoke City
wametoa dau la pauni milioni 16 kutaka kumsajili mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 22,
na wako tayari kumlipa pauni 70,000 kwa wiki (Mirror), Burnley wanataka kumfanya beki Michael
Keane, 23, kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu hiyo ili kuzuia kusajiliwa na
Leicester City (Mirror), mchezaji wa zamani wa
Arsenal na Manchester United Robin van Persie, 32, anauzwa na klabu yake ya Fernabahce (Evening
Standard), mshambuliaji wa Manchester United
Ashley Fletcher, 20, amekataa mkataba mpya na atafanya vipimo West Ham (Manchester Evening
News).
chz
@Kikeke
Chapisha Maoni