0
Vyombo vya habari vya UTURUKI vimetoa picha
zinazoonyesha watu WATATU waliohusika katika
mashambulio yaliyotokea uwanja wa ndege wa
ATATURK Jumanne iliyopita.
Picha hizo zimewaonesha washambuliaji hao
dakika chache kabla ya kufyatua risasi ovyo katika
uwanja huo ambapo watu 44 wameuawa na zaidi
ya 200 kujeruhiwa.
Vyombo hivyo vya habari vimemuonyesha
mwanaume aliyekuwa na furaha kwenye picha hizo
ambaye inasemekana ni mmoja wa washambuliaji
wa kutumia bomu.
Maafisa serikali wamesema watu hao wanasadikiwa kuwa ni raia wa RUSSIA, UZBEKISTAN na KYRGYZSTAN.

Chapisha Maoni

 
Top