0
Na Lydia Churi, Mahakama ya Tanzania
Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa
Mohamed Chande Othman amewakubali na
kuwaapisha Mawakili wapya 624 na
kuifanya Tanzania kuwa na jumla ya
Mawakili 5800.
Akizungumza na Waandishi wa Habari
wakati wa sherehe za kuwaapisha Mawakili
leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es
salaam, Jaji Mkuu wa Tanzania alisema
mawakili walioapishwa wanatoka katika
maeneo mbalimbali ikiwemo Serikalini,
sekta binafsi, mashirika ya Umma na
halmashari mbalimbali nchini.
Alisema hivi idadi ya Mawakili inaendelea
kuongezeka ambapo mwezi Desemba mwaka
huu Mahakama inatarajia kuwaapisha
mawakili wengine zaidi ya 300. Aliongeza
kuwa kwa upande wa Afrika Mashariki,
Kenya inaongoza kwa kuwa na idadi
kubwa ya mawakili ambapo ina zaidi ya
Mawakili 14,000. Uganda kwa upande wake
inayo mawakili 2500.
Aidha, Jaji Mkuu aliwataka mawakili
walioapishwa leo kutekeleza wajibu wao
katika maeneo matatu ambayo ni
kuwajibika kwa wateja wao kwa
kuhakikisha wanatoa huduma kwa viwango
vya kuridhisha.
Aliyataja maeneo mengine mawakili hao
wanayopaswa kutekeleza wajibu wao kwa
ni kwa mahakama ya Tanzania pamoja na
kuwajibika kwa taaluma yao kwa
kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa
kuzingatia maadili ya taaluma hiyo.
Akizungumzia hatua ya mawakili wengi
kufanya kazi zao maeneo ya mijini zaidi
kuliko maeneo mengine, Jaji Mkuu alisema
hatua hiyo inatokana na sababu za
kiuchumi zaidi ingawa baadhi ya mawakili
walioapishwa leo wanatarajia kwenda
kufanya kazi ya kutoa msaada wa kisheria
katika mikoa mbalimbali nchini na wengine
ni wale walioajiriwa na halmashari
mbalimbali nchini.
Sherehe za kuwakubali na kuwaapisha
Mawakili zimefanyika kwa mara ya 54
tangu kuanzishwa kwa sherehe hizo mwaka 1986 hapa nchini.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top