0
WAKAWAKATI Mahakama Maalumu ya Ufisadi na
Uhujumu Uchumi ikitarajiwa kuanza wakati
wowote, majengo ya mahakama hiyo yanatarajiwa
kukabidhiwa keshokutwa jumatatu.
Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande, alisema
jana kuwa mkandarasi aliyekabidhiwa kazi ya
kukarabati majengo hayo yaliyopo katika Shule
Kuu ya Sheria, pembeni mwa kituo cha mabasi
cha Simu 2000, Ubungo Dar es Salaam, yako
katika hatua za mwisho za ukarabati.
Akizungumza katika viwanja vya Karimjee baada
ya kuapisha mawakili wapya 623 wa Mahakama
Kuu, Jaji Chande alisema tayari Bunge
limeshapitisha muswada wa sheria ya uanzishwaji
wa mahakama hiyo.
Alisema kwa sasa muswada huo utawasilishwa
kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa ajili ya kuusaini ili uwe sheria, kisha sheria
hiyo itatangazwa katika gazeti la Serikali ili
kuruhusu shughuli za mahakama hiyo kuanza.
Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama iko tayari
kuendesha Divisheni hiyo ya Mahakama na baada
ya kukabidhiwa majengo hayo, wataanza kutoa
semina kwa majaji na watumishi wengine wa
mahakama hiyo, kuhusu divisheni hiyo
itakavyoendesha shughuli zake.
Aliweka wazi kuwa mpaka sasa hakuna kesi hata
moja iliyokwishatambuliwa kwamba
itashughulikiwa na mahakama hiyo.ya Ufisadi na Uhujumu Uchumi ikitarajiwa kuanza wakati wowote, majengo ya mahakama hiyo yanatarajiwa
kukabidhiwa keshokutwa jumatatu.
Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chuande, alisema
jana kuwa mkandarasi aliyekabidhiwa kazi ya
kukarabati majengo hayo yaliyopo katika Shule
Kuu ya Sheria, pembeni mwa kituo cha mabasi
cha Simu 2000, Ubungo Dar es Salaam, yako
katika hatua za mwisho za ukarabati.
Akizungumza katika viwanja vya Karimjee baada
ya kuapisha mawakili wapya 623 wa Mahakama
Kuu, Jaji Chande alisema tayari Bunge
limeshapitisha muswada wa sheria ya uanzishwaji
wa mahakama hiyo.
Alisema kwa sasa muswada huo utawasilishwa
kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa ajili ya kuusaini ili uwe sheria, kisha sheria
hiyo itatangazwa katika gazeti la Serikali ili
kuruhusu shughuli za mahakama hiyo kuanza.
Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama iko tayari
kuendesha Divisheni hiyo ya Mahakama na baada
ya kukabidhiwa majengo hayo, wataanza kutoa
semina kwa majaji na watumishi wengine wa
mahakama hiyo, kuhusu divisheni hiyo
itakavyoendesha shughuli zake.
Aliweka wazi kuwa mpaka sasa hakuna kesi hata
moja iliyokwishatambuliwa kwamba
itashughulikiwa na mahakama hiyo.

Chapisha Maoni

Top