0
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart & Co
imeifungia kampuni ya Mkono & Company
Advocate kwa kushindwa kulipa malimbikizo ya kodi inayofikia Sh1 bilioni.
Kampuni hiyo inahusishwa na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM) ambaye pia
ni wakili maarufu nchini.
Hata hivyo, Mkono hakupatikana mara moja kuzungumzia suala hilo. Hati ya TRA iliyosainiwa
na Kamishna wa TRA, Neema Mrema imesema Yono imepewa mamlaka na Kamishina Mkuu wa mamlaka hiyo chini ya kifungu cha 64 cha Sheria
ya Kodi ya mwaka 2015 ya kushika mali za mdaiwa anayeshindwa kulipa kodi.
“Naomba kupata usaidizi wa Yono Auction Mart &
Company Ltd na Polisi kutaifisha na kuhamisha bidhaa na mali popote zilipo ili kwa njia yoyote zikiuzwa zilipe deni jumla ya Sh1,101,432,045.99
pamoja na gharama za wito uliotolewa chini ya
Kamishna….” ilisema sehemu ya hati hiyo.
Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Yono
Auction Mart Co. Ltd, Stanley Yono alikiri
kuifungia kampuni hiyo mpaka itakapolipa deni
hilo.
“Ni kweli tumeifungia kampuni ya uwakili ya Mkono na hapa tuko kwenye eneo la tukio.
Anadaiwa zaidi ya Sh1 bilioni ikiwa ni
malimbikizo ya VAT (Kodi ya Ongezeko la Thamani), kodi za mishahara na nyinginezo kwa
mwaka mzima. Amegoma kutia saini hii hati
lakini haitasaidia kitu kwani tumeshamfungia,” alisema Yono.
Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa kodi
wa TRA, Richard Kayombo alikiri kuifungia kampuni hiyo.






Mpekuzi blog

Chapisha Maoni

 
Top