0

Walcott amefunga magoli mawili kwa mara ya
kwanza katika mechi moja ya UEFA tangu Oktoba
2007 alipofanya hivyo dhidi ya Slavia Prague
Magoli mawili ya winga wa Arsenal Theo Walcott
kwenye mchezo wa Kundi A michuano ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya UEFA dhidi Basel yamemfanya
atengeneze rekodi yake kwenye michuano hiyo
mikubwa barani Ulaya kwa ngazi ya klabu.
Nyota huyo wa Uingereza amefunga goli lake la
kichwa kwa mara ya kwanza katika michuano ya
hiyo ya Ulaya.
Walcott amefunga magoli mawili kwa mara ya
kwanza katika mechi moja ya UEFA tangu Oktoba
2007 alipofanya hivyo dhidi ya Slavia Prague.
Matokeo hayo yamewafanya vijana wa Wenger
kucheza mechi nane bila kupoteza kwenye
mashindano yote tangu walipochezea kipigo
mbele ya Liverpool siku ya ufunguzi wa ligi Kuu
ya Uingereza.
Ushindi wa Arsenal dhidi ya Basel ni ushindi wa
kwanza msimu huu kwenye michuano hiyo baada
ya kutoka sare katika mchezo wao wa kwanza
dhidi ya PSG.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top