Supastaa huyo wa United mwenye umri wa miaka
23 amezidi kuimarika katika kila mechi
anayocheza akiwa na Mashetani Wekundu
Licha ya kiwango kisichoridhisha cha Mashetani
Wekundu dhidi ya Zorya Luhansk katika mechi
yao ya Ligi ya Uropa Alhamisi, takwimu mpya
zinaonesha kuwa Paul Pogba alicheza katika
kiwango kikubwa.
Mchezaji huyo ghali zaidi duniani alikuwa
muasisi wa mlolongo wa pasi katika safu ya
kiungo licha ya kutoleta madhara ndani ya eneo
la hatari la wapinzani.
Marouane Fellaini alicheza eneo la kati Pogba
alipocheza kama mchezaji asiye na majukumu,
na takwimu zimeoneysha hasa ubora wa
Mfaransa huyo.
Kwa mujibu wa kampuni ya data za soka Opta,
mkali huyo alipiga pasi 107 zilizokamilika dhidi
ya miamba wa Ukraine; pasi nyingi zaidi akiwa
na United.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni