Alhamisi usiku Manchester United iliichapa Zorya
Luhansk bao 1-0 katika mchezo wake wa pili wa
ligi ya europa, mchezo uliopigwa kwenye dimba la
Old Trafford.
Bao pekee la United liliwekwa kambani kwa kichwa
na Zlatan Ibrahimovic hilo likiwa ni bao lake la sita
tangu ajiunge na United wakati wa usajili wa majira
ya joto.
Licha ya kutawala mchezo huo, United imeshindwa
kupata ushindi mnono, Zorya ilitumia zaidi mchezo
wa kujihami na 'kubaki basi.'
Nayo KRC Genk anayocheza Mtanzania Mbwana
Samatta ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya
Sassuolo katika moja ya michezo mingine ya ligi
hiyo.
Samatta alianzia benchi katika mpambano huo.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni