0
Kocha Mkuu wa Timu ya ‘Wachimba
Almas’ Mwadui FC, Ally Bushiri
amezitaja Mechi mbili zilizosalia kati
ya Simba SC na Azam FC kuwa ndio
mechi muhimu zaidi msimu huu
kwani zinaweza kumjengea Heshima
vizuri anapoenda kumaliza Msimu wa
2016/17.
Kocha huyo ambaye amewahi
kuzifundisha timu ya KMKM ya
Zanzibar pamoja na kuwapo katika
Benchi la Ufundi la Taifa Stars kipindi
cha kocha Marcio Maximo amesema
licha ya kwamba wapo sehemu
salama lakini Kuzifunga Timu hizo
itamjengea Heshima katika tasnia ya
Soka.
-Najua tumebakiwa na mechi ngumu
dhidi ya Simba na Azam, ila
tutapambana kuhakikisha tunamaliza
kwa ushindi ili tuweze kujiweka
kwenye mazingira mazuri zaidi’
Bushiri aliuambia Mtandao huu.
Wachezaji wanaweza.
Kocha huyo mkongwe ambaye
alichukua mikoba ya Kocha Jamhuri
Kihwelu Julio wakati Mwadui wakiwa
katika nafasi ya 15 ya msimamo wa
Ligi kuu Soka Tanzania Bara amesema
kikubwa ili kushinda mchezo huo ni
kuwatengeza wachezaji wake wawe
katika moyo wa ushindani.
-Tumetoka kupoteza dhidi ya Majimaji
kwa Mabao 3-0 sasa kama mwalimu
najua wachezaji wanaweza kutishika
kidogo lakini, Kikubwa naendelea
kuwajenga wachezaji wangu kwamba
wanaweza na wataweza kuwafunga
hao Azam na Baadae Simba"
Aliongeza.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top