
Kwenye Mechi ya mapema huko Anfield Jijini Liverpool, walikosa nafasi safi ya kushinda baada ya Penati ya Kipindi cha Pili ya James Milner kuokolewa na Kipa wa Southampton Fraser Forster.
Kisha ikafuata Mechi ya huko Emirates kati ya Arsenal na Man United iliyobadili Kikosi chake Wachezaji 8 na pia kumtumia ChipukiziI a Miaka 19, Tuanzebe, aliekuwa akicheza
Mechi yake ya kwanza kabisa kwa Kikosi cha Kwanza huku pia ikimwingiza mpya mwingine McTominay kwenye Kipindi cha Pili.
Kabla ya Mechi hii, Jose Mourinho alidokeza kuweka mkazo kwenye UEFA EUROPA LIGI ambako Majuzi Alhamisi waliichapa Celta Vigo 1-0 huko Spain kwenye Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali na Alhamisi hii kurudiana huko Old Trafford.
Mshindi wa UEFA EUROPA LIGI hucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimi ujao.
Bao za Arsenal hii Leo zilifungwa Kipindi cha Pili Dakika za 54 na 57 na Granit Xhaka na Danny Welbeck.
Matokeo ya Leo yameiacha Chelsea ikiongoza Ligi ikiwa na Pointi 81 kwa Mechi 34 wakifuata Tottenham wenye Pointi 77 kwa Mechi 35, Liverpool ni wa 3 na wana Pointi 70 kwa Mechi 36, kisha Man City waliocheza Mechi 35 na wana Pointi 65.
Man United wamecheza Mechi 35 na wana Pointi 65 wakishika Nafasi ya 5 wakifuata Arsenal waliocheza Mechi 34 na wana Pointi 63.
EPL, LIGI KUU ENGLAND Ratiba:
Jumatatu Mei 8
2200 Chelsea v Middlesbrough
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.