Msimbazi Simba SC Jackson Mayanja
Raia wa Uganda amesema mchezo wa
fainali ya Azam Sports Federation Cup
dhidi ya Mbao FC ni Kama mchezo wa
kumaliza msimu wa 2016/17.
Mayanja amesema hawana budi
kujipongeza kwa kufika hatua hiyo na
kwamba anatarajia mchezo wa Ufundi
kwa timu zote mbili, mchezo ambao
utafanyika Katika uwanja wa Jamhuri
mkoani Dodoma.
-Kwanza kabisa Kesho Ndio
tunamaliza msimu, ligi
imekwishamalizika na huu Ndio
mchezo pekee wa kuhitimisha msimu,
Nawapongeza wale Wote ambao
wamefikia hatua Hii, tunatarajia kuona
mchezo mzuri' Amesema Mayanja.
Pongezi kwa DOREFA.
Katika hatua nyingine Mayanja
amekipongeza Chama cha Soka Mkoa
wa Dodoma DOREFA kwa kufanya
Maandalizi mazuri ya Mchezo huo
ambapo amekiri kwamba Maandalizi ni
mazuri.
-Nawapongeza sana chama cha Soka
mkoani hapa kwa kazi yao, tumefika
Jana na tumepokelewa vizuri, naona
kabisa wamejipanga na kujiandaa
vizuri tunasubiri siku ifike ili tujue
tumevuna nini" Mayanja aliongeza.
Kuhusu kikosi kinachotarajiwa
kucheza kesho, Mayanja amewatoa
hofu mashabiki wa Simba na
kuwaambia kuwa kikosi Kipo katika
Hali nzuri na watarajie mchezo Mzuri.
Mayanja ameyasema hayo wakati wa
mkutano na waandishi wa habari
kuelekea katika mchezo wa Fainali ya
Kombe la Shirikisho Tanzania Bara,
Jumamosi ya Mei 27 Mjini Dodoma.

Chapisha Maoni