ya umri wa miaka 17,
Serengeti Boys leo
imefungwa 1-0 na wenyeji
Cameroon katika mchezo wa
kirafiki mjini Yaounde,
Cameroon.
Kipigo hicho ni sawa na
kisasi, baada ya Serengeti
Boys kuifunga Cameroon 1-0
Aprili 30 katika mchezo
mwingine wa kujipima
nguvu.
Siku hiyo, bao la Serengeti
Boys lilifungwa na Ally
Ng'anzi dakika ya 36 katika
mchezo ambao ulihudhuriwa
na gwiji wa soka wa
Cameroon, Rogger Milla.
Serengeti Boys ilitua Younde,
Cameroon Alhamisi iliyopita
ikitokea mjini Rabat, Morocco
ambako iliweka kambi ya
karibu mwezi mmoja na
kucheza mechi mbili za
kirafiki dhidi ya Gabon na
kushinda 2-1 kila mchezo.
Kwa ujumla Serengeti Boys
imekwishacheza mechi sita
tangu kuanza kambi rasmi ya
maandalizi fainali za Gabon,
baada ya awali kuifunga
Burundi mara mbili, Machi 30
mabao 3-0 na Aprili 1 mabao
2-0, mechi zote mbili
zikipigwa Uwanja wa Kaitaba,
Bukoba, kabla ya
kulazimishwa sare ya 2-2 na
Ghana ‘Black Starlets’ Aprili
3 Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Baada ya mchezo wa leo,
Serengeti Boys inatarajiwa
kuendelea na mazoezi katika
kambi yake ya wiki moja
Cameroon, kabla ya Mei 7
kwenda Gabon ambako
imepangwa kundi B pamoja
na timu za Mali, Niger na
Angola.
Cameroon nayo itashiriki
fainali hizo ikiwa imepangwa
Kundi A lina timu za wenyeji,
Gabon, Guinea na Ghana.
Chapisha Maoni