Hatua ya Kocha, Pep
Guadiola kusafisha wachezaji wenye umri mkubwa klabu hapo, inaonekana kushika
kasi baada ya mchezaji Bacary Sagna kuthibithwa kwamba anaondoka kikisoni hapo.
Taarifa ya kuondoka mchezaji huyo iliwekwa kwenye tovuti ya klabu hiyo jana Alhamisi.
Sagna anafanya idadi ya wachezaji waliothibitishwa kuachana na kikosi hicho kufikia wanne. Wachezaji wengine ni Gael Clichy, Jesus Navas na Willy Caballero.
Hivi karibuni kulikuwapo na tetesi za kuondoka mkongwe, Yaya Toure anayeonekana kusubiri uamuzi wa kocha
iwapo atahitaji huduma yake msimu ujao au la.
ôNimefurahia maisha ya soka muda wote nilipokuwa na Manchester City.
Ninawashukuru wafanyakazi wote klabuni pamoja na wachezaji wenzangu
kwa miaka yote mitatu niliyokuwapo, wamenipa ushirikiano mkubwa, alisema
Sagna.
Awali, Sagna aliitumikia Arsenal kwa miaka saba kabla ya kujiunga na Manchester City mwaka 2014. Msimu huo aliiwezesha klabu yake kutwaa taji moja.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni