0

Simba imetwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Azam kwa kuifunga Mbao kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na kufuzu kucheza Kombe la Shirikisho Afrika
mwakani.
Simba ilipata mabao yake mawili yaliyofungwa na washambuliaji wake Fredrick Blagnon na penalti ya Shiza Kichuya wakati bao la kufutia machozi kwa Mbao lilifungwa na Ndaki Robert.
Katika mchezo huo wa fainali timu zote mbili zilicheza kwa nguvu na kujilinda kwa umakini hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika timu hizo zilikuwa suruhu.
Kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko lakini uamuzi wa Joseph Omog kumtoa Said Ndemla dakika 83 na kuingia Fredrick Blagnon uliokuwa ni
habari njema kwa Simba.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alifungia Simba bao la kwanza katika dakika 95, lakini Mbao ilisawazisha dakika 109 kupitia Ndaki.
Wakati mashabiki wakiamini mechi hiyo itakwenda kwenye penalti katika dakika 116, uamuzi wa utata wa mwamuzi Mohamed Kikumbo ulifaidisha Simba kwa kupata penalti.
Uamuzi ulisababisha wachezaji wa Mbao kumvaa mwamuzi Kikumbo wakipinga uamuzi huo na kusababisha askari kuingia uwanjani kutuliza
ghasia.
Baada ya vurugu hizo mpira uliendelea kwa Kichuya kupiga penalti hiyo na kuifungia Simba bao la pili na ushindi na kuamsha shangwe uwanjani hapo.
Awali milango ya Uwanja wa Jamhuri ulifungwa saa 8.00 mchana baada ya majukwaa yote kujaa.
Ukikadiriwa kutimiza idadi ya mashabiki 23,000 idadi iliyotangazwa na shirikisho la soka Tanzania (TFF) na chama cha soka Dodoma (Dorefa)
Kitendo cha timu ya Simba kutoonekana wakishuka kwenye basi uwanjani kimeonekana kuwashangaza mashabiki wengi waliofika kutazama pambano hili la fainali.
Mchezo huo unaochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma umevuta hisia nyingi za mashabiki waliofurika na kujaza uwanja huu.
Lakini katika hali isiyotarajiwa na wengi basi la timu ya Simba SC lililoingia uwanjani lilikua tupu na waliokua ndani yake ni wachezaji wanne pekee.


Chapisha Maoni

 
Top