kutoka Jijijii Mwanza umelaumu
Shirikisho la Soka NchiNI (TFF) kwa
kushindwa kuwathibiti waamuzi wa
soka nchini kufanya maamuzi ya haki
na kusema kuwa kama wataendelea
kufanya maamuzi yasiyozingatia
kanuni 17 za mpira wa miguu basi
Tanzania itaendelea kufanya vibaya
katika michuano ya kimataifa kwa
kuwakilishwa na timu ambazo
hazikufuzu kihalali lakini kwa
kubebwa.
Akizungumza na futaa.co.tz msemaji
wa Mbao Fc Klisant Malinzi ambaye
timu yake imeshindwa kwamabao 2-1
na Simba amesema kuwa Tmu yake
ilikuwa na uwezo wa kushinda
mchezo huo lakini hawakutendewa
haki kwa kunyimwa penati mbili
ambazo amezitaja kuwa za wazi.
Tumenyimwa penati
-Kilichotokea uwanjani ni kitu cha
aibu katika soka la nchi hii kila mtu
aliona waliokuwa uwanjani na
waliokuwa wakiangalia kwa runinga
tumepata penati mbili wameangusha
wachezaji wetu wawili kwenye penati
box lakini refa hakuchukua hatua,lakini
sisi beki wetu ametoa mpira kwenye
eneo la hatari refa akalazimisha
penati.
Aidha Malinzi ameendelea na kusema
kuwa kama soka la Tanzania
litaendelea kuendeshwa kwa hali hiyo
Tanzania itaendelea kupata matokeo
mabaya katika mashindano ya
kimataifa.
Waakilishi wasio halali
-Kama bingwa anapatikana kwa
kulazimishwa hivi kwa kuchaguliwa na
muamuzi uwanjani bila matokeo halali
ya uwanjani tutazidi kupata
matwaakilishi ambao sio halali kabisa
na ndio maana tunapata aibu
tunafungwa tunarudi nchini,ni aibu
tumefungwa kwa kulazimishwa lakini
sisi ndio tulistahili kuwa mabingwa wa
Kombe hilo”,ameongeza Malinzi.
Pamoja na kupokea zawadi ya shilingi
milioni 50 Simba pia watapata fursa
kuwakilisha Tanzania kwenye
michuano ya Kombe la Shirikisho
barani.

Chapisha Maoni