Mkufunzi wa Arsenal ametaja ukosoaji ambao amekuwa akipata msimu huu kuwa hujuma ambayo hatosahau.
Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 67
amekabaliwa na shutuma kali kutoka kwa mashabiki kwa kumtaka kuondoka katika klabu hiyo ambayo ameingoza tangu 1996.
''Sijali ukosoaji kwa sababu tunafanya kazi ya umma'', aliambia BBC kabla ya mechi ya fainali kati ya Arsenal na Chelsea katika uwanja wa
Wembley.
''Ninaamini kuna tofauti kati ya kukosolewa na kuchukuliwa hali ambayo hairuhusu kwa
mwanadamu''.
Aliongezea: Utovu wa heshima kutoka kwa baadhi umekuwa hujuma na sitokubali.Sitosahau.Tabia ya
baadhi ya watu msimu huu, ndio kitu kinachoniuma sana. Sio mtu wangu ambaye
ameathiriwa lakini sura ya klabu hii duniani.Tabia
hiyo haionyeshi tabia ya Arsenal.
''Klabu kilichoimarika ni kile kinafanya maamuzi . Ni makosa kwamba katika kizazi kipya sio swali la iwapo uamuzi ni sawa lakini iwapo ni maarufu.Hilo halifai kufananishwa na uwezo wa mtu.Watu wenye majukumu lazima wafanye uamuzi wa sawa''.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni