FC ‘Wabishi’, wamejitokeza kuulaki
msafara wa Timu hiyo uliokuwa
ukitoka Mkoani Dodoma Kucheza
mchezo wa Fainali ya Kombe la
Shirikisho dhidi Simba.
Mashabiki hao wakiongozwa na
Mwenyekiti wa Soko la Mbao lililopo
Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza John
Masumbuko, bila kujali mvua
iliyokuwa ikinyesha walijumuika
pamoja kulisindikiza basi lililobeba
Mashabiki kwa zaidi ya Kilomita 16
kutoka Nyegezi.
Akizungumza na Umati wa Mashabiki
waliojitokeza kuwapokea wachezaji
hao, John Masumbuko aliwataja
wachezaji hao kama wapiganaji
ambao wameutangaza Vyema mkoa
wa Mwanza kwa kufika hadi hatua
hiyo ya Fainali.
-Wanasema wapiganaji kuna mambo
mawili, kushindwa na kushinda, lakini
hii ya kwetu haikuwa kushindwa
zilikuwa ni mbinu tu ambazo
zimetumika ili watu waweze
kujiridhisha, nyie ni wapiganaji
Hongereni kwa Hilo’ Alisema
Masumbuko.
Tumeshangaa.
Aidha kwa Upande wa Nahodha wa
Kikosi cha Mbao Yusufu Ndikumana
ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa
wachezaji wenzake wakiwa Uwanjani,
amewashukuru mashabiki wote
waliojitokeza kuwapokea licha ya
kufungwa na Simba katika Mchezo
huo.
-Nashukuru sana kuona mmetufanyia
mambo kama haya, yani hatukuwa
tunategemea kama tutapokelewa hivi,
tunashuruku sana na Mungu
awabariki, nafikiri kama Msimu ujao
tutakuwa na mshikamano kama huu
msimu ujao tutazidi kufanya Vizuri’
Nahodha Ndikumana Alisema.
Mbao wanarejea Jijini Mwanza kama
Makamu Bingwa wa Azam Sports
Federations kwani walipoteza katika
mchezo wa Fainali kwa Mabao 2-1,
mabao ambayo yalipatikana katika
dakika 30 za Nyingeza baada ya
dakika 90 kumalizika kwa Sare ya
0-0.

Chapisha Maoni