0
Mwenyekiti wa Klabu ya Stand United
‘Chama la Wana’ Ellyson Maeja,
amekiri wazi wazi kuwa Wachezaji wa
Timu hiyo wameondoka Kambini bila
ya Kulipwa mishahara yao, na
kwamba wanatafuta namna ya kuweza
kuwalipa kadri watakavyopata.
Maeja amesema Tatizo la Stand
United si la kwao peke yao na
kwamba Watakapo pata Pesa basi
watawajibika kuwalipa wachezaji wote
ambao wanadai Mishahara kwani
itakuwa ni dhambi kubwa kutowalipa
watu waliyoisaidia Timu kufika hapo
ilipo.
-Nakiri kabisa nah ii si kwa Stand tu!,
ni Timu nyingi ulishawahi kusikia
Timu kama Simba na Yanga
wachezaji hawajalipwa miezi miwili
wengine Mitatu, sisi mpaka tunamaliza
ligi wachezaji walikuwa wanatudai
mishahara ya miezi miwili, kwa hiyo
wameondoka pindi tutakapopata pesa
Tutawalipa Mishahara yao’ Alieleza
Maeja.
Ikumbukwe kwamba Timu ya Stand
United iliwahi kuwa na mkataba
Mnono wa udhamini na kampuni ya
uchimbaji madini ya ACACIA, wa
Takribani Bilioni 2.4 lakini migogoro
ndani ya Klabu hiyo iliwakimbiza
wadhamini hao mwanzoni mwa Msimu
uliopita hali ambayo ikaifanya Stand
United kuwa dhohofu hasa katika
Masuala ya kiuchumi.
Aidha Katika Msimamo wa Ligi
iliyomalizika hivi karibuni Stand
United walimaliza nafasi ya Sita
wakiwa na alama 38, wakifunga
mabao 25, huku wakiruhusu nyavu
zao kuguswa zaidi ya Mara 23.

Chapisha Maoni

 
Top