Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania 'Taifa Stars' inatarajiwa kuweka kambi
nchini Misri kujiandaa na Mchezo wa Kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika mwaka 2019 nchi Cameroon.
Akizungumza na Mtandao huu Meneja wa Taifa Stars Danny Msangi amesema kikosi hicho kitaondoka kuelekea Misri Mei 30 kuweka kambi ya Muda Mfupi Kabla ya kurejea tena
Jijini Dar es Salaam tayari kwa
mchezo huo. -Tayari wachezaji wote kasoro Jonas Mkude wamekwishafika kambini na
Timu inatarajiwa kuondoka Mei 30 kwa ajili ya Kambi hiyo fupi kujiandaa na Mchezo dhidi ya Lesotho Juni 10 Mwaka huu" Alisema.
-Wachezaji wote wanaocheza ligi ya Ndani tayari wamekwisharipoti ambapo wachezaji wa Simba Ndio
walikuwa wa Mwisho kuripoti, Lakini Bahati Mbaya Mkude wakati anakuja kujiunga na wenzake alipata ajali,
tunamuombea apate ahueni na
kujiunga na wenzake". Alieleza
Msangi.
Tanzania imepangwa katika kundi L ikiwa pamoja na Uganda, Lesotho na Cape Verde, ambapo watacheza
mchezo wa kwanza dhidi ya Lesotho Juni 10 Jijini Dar es Salaam.
Nyumbani
»
Sport News
» Taifa Stars kuweka kabi yao Misre kwa Mafarao Kabla ya mchezo wao dhidi
ya Lesotho.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni