0

Nahodha wa klabu ya Manchester United Wayne
Rooney anasema kuwa bado hajaamua kuhusu hatma yake katika klabu hiyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 hajachezeshwa sana msimu huu huku akiingia
kama mchezaji wa ziada katika kombe la ligi ya Yuropa dhidi ya Ajax.
''Kuna maombi mengi mezani, Uingereza na ughaibuni'', alisema.
Rooney ambaye anaongoza kwa mabao 253 amesema kuwa angehamia Everton iwapo
angesalia katika ligi ya Uingereza.
Inaaminika kwamba Rooney hataki swala la kandarasi yake mpya kuchukua muda mrefu hadi siku ya mwisho ya uhamisho mnamo tarehe 31
Agosti ,na ataondoka na familia yake kujadiliana na kuamua kuhusu hatua atakayochukua.
Rooney amesema kwamba hawezi kuichezea klabu
nyengine yoyote katika ligi ya Uingereza isipokuwa
Everton, huku meneja wa Toffees, Ronald Koeman
na mkurugenzi wa soka Steve Walch wakisema wazi msimu huu kwamba wangemtaka mchezaji huyo iwapo atapatikana.
Rooney alijiunga na klabu hiyo ya Old Trafford kwa pauni milioni 27, 2004 na amefanikiwa kucheza
takriban mechi 500 na kuvunja rekodi iliowekwa na Sir Bobby Charlton ya miaka 44 kwa kufunga mabao mengi msimu huu.


Chapisha Maoni

 
Top