Mabingwa wa taji la Europa ligi msimu huu klabu ya Manchester United inatarajiwa kuweka kikomo cha kufanya usajili kwa wachezaji watatu au
wanne muhimu katika dirisha kubwa la usajili Meneja wa United Jose Mourinho amesema makamu mwenyekiti wa timu hiyo Ed Woodward
anajua wachezaji wanaotakiwa kwa zaidi ya miezi miwili iliyopita.
"Ed Woodward anayolisti yangu ya wachezaji ninaowataka ," alisema meneja huyo baada ya
mchezo wa Europa ligi dhidi ya Ajax .
Mourinho anataka kuongeza changamoto katika safu ya ulinzi na ushambuliaji ili kuweza kuwania taji la ligi kuu ya England msimu ujao.
United wamekua wakihushwa na kutaka kuimarisha
safu ya ushambuliaji kwa kuwasajili Antoine Griezmann toka Atletico Madrid, Andrea Belotti wa Torino pamoja Romelu Lukaku. Kwa Upande wa safu ya ulinzi wachezaji
wanaotajwa kuwa wako kwenye rada ya Mourinho
ni beki wao wa zamani Michael Keane anayechezea Burnley,beki kisiki wa Benfica Victor Lindelof na Muholanzi Virgil van. Dijk wa Southampton.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni