Kocha Athuman Bilal Maarufu kama ‘Bilo’, anatarajia kuongeza mkataba wa kuendelea kuifundisha Timu ya Stand United ‘Chama la Wana’ baada ya kuisadia Timu hiyo kusalia katika Mikimiki ya Ligi kuu soka Tanzania Bara.
Mchezaji huyo wa zamani wa Kurugenzi ya Kigoma, Biashara ya Shinyanga, Pamba Fc ya Mwanza na Vital’o ya Burundi anatarajia kuongeza mkataba wa mwaka mmoja utakaofanya kuwa kocha mkuu wa Standa United licha ya kukataa tetesi hizo.
-Mungu akipenda Siku ya Jumatano au Alhamis kila kitu kitakaa sawa na nitasaini Mkataba Mpya na Stand United, kila kitu kikishakamilika basi nitaweka mambo yote hadharani ili kila Mtanzania afahamu” Alisema.
Hakuna Kitakachoharibika.
Amesema kwamba kila siku anafanya mawasiliano na uongozi wa klabu hivyo anaamini kabisa kuwa kila ambacho wamekizungumza na kukubaliana kitakuwapo katika Mkataba anaotarajia kusaini.
-Kila siku ninakuwa na mawasiliano na uongozi , hata tulipomaliza ligi kuna kozi moja ilifanyika pale Morogoro uongozi huohuo ukanilipia baadhi ya gharama ukanipeleka hivyo naamini kabisa hakuna kitu kitakachoshindikana katika Mkataba wetu’ Alieleza.
Bilal ambaye msimu uliopita alikuwa kocha msaidizi chini ya Makocha wawili Mfaransa Patrick Lewing na Mzanzibar Hemed Moroko kabla ya kukabidhiwa timu rasmi ikiwa imebaki takribani michezo mitano aliisaidia kumaliza nafasi ya sita wakiwa na alama 38.
Chapisha Maoni