Nyota wa Zamani wa Timu ya Taifa Stars na Timu ya Simba SC ya Jijini Dar es Salaam Boniface Pawasa amewaomba Simba kuhakikisha wanamalizana na Kiungo Haruna Niyonzima kama kweli wanamuhitaji.
Akizungumza na Kituo cha Luninga cha ITV, Pawasa Aliwashauri Simba kukamilisha dili hilo Mapema zaidi kwani Niyonzima ni miongoni mwa viungo bora ambao kama Simba watamnasa Basi watakuwa Wameramba dume.
-Nakiri kabisa Niyonzima ni Kiungo Mzuri sana na mchezaji muhimu Sana kuwapo katika Timu, Nawashauri Simba kama kweli wanamuhitaji Basi wachukue Mapema ili wajenge kikosi" Alisema Pawasa.
Kuhusu Ibrahim Ajib.
Kuhusu uhamisho wa Mshambualiaji Ibrahim Ajib kuhusishwa na kujiunga Yanga, Pawasa amesema litakuwa pigo kwa Simba kumkosa Lakini Anataka kuondoka basi hakuna namna zaidi ya kumruhusu.
-Ajib ni mchezaji mzuri sana, Ila Kwa sasa amekuwa na majukumu Mengi Kama utakumbuka ameoa juzi tu hapo na Anataka kujenga maisha yake, kwa hiyo Naamini ataenda kwenye timu ambayo itakuwa na maslahi makubwa kwake, Kama ataondoka Simba litakuwa ni pigo Lakini hakuna namna kama atakuwa anajenga maisha yake" Pawasa Alisema.
Chapisha Maoni