0
Ripoti zinadai kuwa Arsenal wanaandaa dau la paundi milioni 54 kwa ajili ya Alexandre Lacazette, licha ya rais wa Lyon kusisitiza mchezaji huyo hauzwi
Mshambuliaji wa Lyon anaonekana shabaha kuu ya Arsenal majira ya joto, ingawa rais wa Lyon, Jean-Michael Aulas, amesema bado hajapokea ofa yoyote. Lakini Daily Star limedai kuwa Arsenal wapo mbioni kutoa ofa ya paundi milioni 54 kwa ajili ya mchezaji huyo.
Lacazete alikuwa karibu kujiunga na Atletico Madrid kama mrithi wa Antoine Griezmann kabla ya dili hilo kushindikana baada ya Atletico kufungiwa usajili, na imeripotiwa Manchester United, Liverpool na Borussia Dortmund zinavutiwa naye pia.
Mashabiki weingi wanasubiri kwa hamu kuona Arsenal ikimsajili. Lacazette ni miongoni mwa washambulizi wanaopewa nafasi kubwa kutua Emirates kutokana na kiwango chake kizuri msimu uliopita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amefunga mabao 28 katika mechi 30 za Ligue 1 akiwa na Lyon msimu wa 2016/17 na kuisaidia timu yake kutinga nusu fainali michuano ya Europa.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top